Kwa sasa kuna watu wengi ambao huamini kwa njia ya rabsha. Udadisi wenu ni mkubwa mno, tamaa yenu ya kufuatilia baraka ni kubwa mno, na hamu yenu ya kufuatilia maisha ni ndogo mno. Waumini katika Yesu siku hizi wamejaa shauku. Yesu atawakaribisha katika nyumba ya mbinguni–je, wao hawawezi kuamini? Watu wengine ni waumini katika maisha yao yote, wameamini kwa miaka arobaini au hamsini, na hawachoki kamwe kusoma Biblia. Hii ni kwa sababu bila kujali kinachotokea, mradi wao wanaamini, wataingia mbinguni. Mmemfuata Mungu kwa njia hii kwa miaka michache tu, lakini tayari mnajitahidi sana na hamna uvumilivu tena.
Hii ni kwa sababu hamu yenu ya kupata baraka ina nguvu mno. Nyinyi kuitembea njia hii ya kweli kunadhibitiwa na hamu yenu ya kupata baraka na nyoyo zenu chunguzi. Hamna ufahamu mwingi wa hatua hii ya kazi. Mengi ya yale Ninayoyasema leo siyo kuongea kwa wale watu wanaoamini katika Yesu; hayaongewi hata kidogo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao. Kwa kweli, hizi dhana zinazofichuliwa ni dhana zile zile ambazo zipo kati yenu, kwa sababu hamuelewi ni kwa nini Biblia imewekwa chini, kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yehova imezeeka, na kwa nini Ninasema kuwa kazi ya Yesu imezeeka. Kwa kweli, mna dhana nyingi ambazo hamjazipa sauti. Mna dhana nyingi ambazo zimefungiwa ndani ya mioyo yenu, na nyinyi mnafuata umati tu. Je, mnadhani kuwa dhana zenu ni chache? Ni kwamba tu kuwa hamzizungumzii, na hakuna cha ziada! Kwa kweli, mnafuata tu kwa uzembe, hamtafuti njia ya kweli kamwe, na kwa makusudi hamji kupata uzima. Mna mtazamo wa kutaka tu kuona kitakachotokea. Kwa sababu hamjaziacha dhana zenu za zamani, hakuna yeyote kati yenu ambaye ameweza kujitoa mwenyewe kikamilifu. Baada ya kufika wakati huu, nyote mna wasiwasi kuhusu majaliwa yenu wenyewe, mkifikiri mchana na usiku, msiweze kuyaweka chini kamwe. Je, unafikiri kuwa Mafarisayo ambao Mimi nawaongelea ni “wazee” katika dini? Je, si nyinyi ni wawakilishi wa Mafarisayo wa kuendelea mbele zaidi wa enzi ya sasa? Je, unafikiri kwamba wale watu Ninaowataja wanaoniangalia Mimi kwa makini dhidi ya Biblia wanarejelea tu wale wataalamu wa Biblia wa nyanja za kidini? Je, unadhani kwamba Ninapozungumza juu ya wale ambao kwa mara nyingine wanamtundika Mungu msalabani Nazungumzia viongozi wa jamii za kidini? Je, si nyinyi ni wahusika bora kabisa ambao mnaigiza wajibu huu? Je, unafikiri kwamba katika maneno yote Ninayoyanena kurudisha pigo dhidi ya dhana za watu ni mzaha kwa wachungaji na wazee wa dini? Si nyinyi pia mmeshiriki katika mambo haya yote? Je, mnafikiri kuwa mna dhana chache tu? Ni kwamba tu nyote mmejifunza kuwa mahiri sana sasa. Hamzungumzii mambo ambayo hamyafahamu ama kusaliti hisia zenu kuyahusu, lakini mioyo yenu ya heshima na mioyo yenu ya utii haipo tu. Kama mnavyoona, kusoma, kuzingatia, na kusubiri ni matendo yenu makuu ya leo. Mmejifunza kuwa mahiri mno. Je! mnajua, hata hivyo, kwamba hii ni aina yenu ya saikolojia ya ujanja? Je, mnafikiri kuwa wakati wa mahiri kwa upande wenu utawasaidia kuepuka kuadibiwa kwa milele? Mmejifunza kuwa wenye “busara” mno! Na baadhi ya watu huniuliza Mimi mambo kama: “Siku moja, wakati watu wa kidini huniuliza, nini, ‘Mbona Mungu wako hajatenda muujiza hata mmoja?’ Ninafaa kuelezea vipi?” Sasa, siyo tu kwamba watu wa dini watauliza mambo kama hayo. Badala yake, ni kwamba huielewi kazi ya leo, na una dhana nyingi mno. Je, bado hujui ni nani Ninayemrejelea Ninapotaja maafisa wa kidini? Unajua Ninawaelezea nani Biblia? Je, hujui ni kwa nani Ninazungumzia wakati Ninapoeleza kwa mifano hatua tatu za kazi? Je, Singesema vitu hivi, mngeridhishwa kwa urahisi hivyo? Je, mngenyenyekea kwa urahisi hivyo? Je, ni rahisi kwenu kushusha hizo dhana za zamani? Hasa wale “watu halisi” ambao hawajawahi kumtii yeyote–je, wangeweza kutii kwa urahisi sana? Najua kwamba ingawa mna daraja ya chini ya ubinadamu, mna ubora duni sana wa tabia, mna akili ambazo hazijakua sana, na hamna historia ndefu za kumwamini Mungu, kwa kweli mna dhana nyingi kabisa, na asili yenu ya kawaida ni ya kutomnyenyekea yeyote kwa wepesi. Leo, hata hivyo, mnaweza kunyenyekea kwa sababu mnalazimishwa na hamjiwezi; Ninyi ni chui-milia katika kizimba cha chuma, bila uwezo wa kutumia ujuzi wenu. Ingekuwa vigumu kuruka hata kama mngekuwa na mabawa. Ingawa hamjapewa baraka, mnataka kufuata unyounyo. Hata hivyo, hii si roho yenu ya “mtu mzuri”, ila ni kwamba mmeangushwa kabisa, na mnataka kuchanganyikiwa. Ni kwamba kazi yote hii imewaangusha kabisa. Ikiwa kungekuwa na chochote ambacho mngeweza kufikia, hamngekuwa watiifu kama mlivyo leo, kwa sababu awali, nyote mlikuwa punda mwitu nyikani. Hivyo kinachosemwa leo hakielekezwi tu kwa watu wa dini na madhehebu mbalimbali, na siyo kurudisha pigo dhidi ya dhana zao; badala yake ni kurudisha pigo dhidi ya dhana zenu.
Hukumu ya haki imeanza. Je, Mungu bado atatumikia kama sadaka ya dhambi kwa watu? Je, Mungu atachukua nafasi ya daktari mkuu kwa watu tena? Je, Mungu hana mamlaka zaidi ya hivi? Kundi la watu tayari limefanywa kamilifu, na tayari wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi. Je, Yeye bado atawafukuza pepo na kuwaponya wagonjwa? Si hili ni jambo la kale? Je, ushuhuda utawezekana kwa kwendelea jinsi hii? Mungu ametundikwa msalabani mara moja, hivyo Atasulubishwa milele? Baada ya kuwafukuza pepo mara moja, Atawafukuza milele? Je, si hili ni sawa na udhalilishaji? Ni wakati tu hatua hii ya kazi inapokuwa juu zaidi kuliko ile ya awali ndipo enzi husonga mbele. Kisha siku za mwisho zitafikiwa, na wakati utakuja ambapo enzi itahitimishwa. Watu wanaofuatilia ukweli kwa hiyo wanapaswa kuzingatia kuwa dhahiri juu ya maono. Huu ndio msingi. Kila wakati Ninapofanya ushirika nanyi kuhusu maono, daima Mimi huona vigubiko vya jicho vya baadhi ya watu vikinyong’onyea na wakianza kushikwa na usingizi, bila kutaka kusikiliza. Wengine huuliza: “Ni kwa nini wewe husikilizi?” Yeye husema, “Hili halisaidii maisha yangu au kuingia kwangu katika hali halisi. Tunachotaka ni njia za matendo.” Wakati Mimi siongei juu ya njia za matendo, na Ninaongea juu ya kazi, anasema, “Punde unapoongea juu ya kazi mimi huanza kushikwa na usingizi.” Sasa Ninaanza kuzungumza juu ya njia za matendo, na anaanza kuchukua muhtasari. Ninaanza tena kuzungumza juu ya kazi hiyo, na anarejelea kutosikiliza. Je, mnajua ni nini mnachopaswa kujiandaa nacho? Jambo moja ni maono juu ya kazi, na jambo jingine ni matendo yako. Lazima ufahamu mambo yote mawili. Kama huna maono katika jitihada zako za kufanya maendeleo katika maisha, basi huna msingi. Kama una njia za matendo tu na huna maono hata kidogo, na huna ufahamu wowote wa kazi ya mpango mzima wa usimamizi, basi wewe ni bure. Lazima uelewe ukweli wa kipengele cha njozi, na kwa ukweli kuhusu matendo, unahitaji kupata njia mwafaka za kutenda mara unapozielewa; unahitaji kutenda kulingana na maneno, na uingie kulingana na hali zako. Maono ndiyo msingi, na usipozingatia hili, hutaweza kufuata hadi mwisho. Unapopitia njia hii, ama utapotea au kuanguka chini na kushindwa. Hakutakuwa na njia ya kufanikiwa! Watu ambao hawana maono makubwa kama msingi wao wanaweza tu kushindwa na si kufanikiwa. Huwezi kusimama imara! Je, unajua kuamini katika Mungu ni nini? Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa kwa kufuata unaweza kumpata Yeye, kwamba kwa kumuona Yeye unaweza kumpata,[a] na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi. Pia, msidhani kwamba katika kuachana na watu wa kidunia ili kuwa watakatifu kwamba nyinyi ni familia ya Mungu. Leo ni Mungu Mwenyewe ambaye anafanya kazi miongoni mwa uumbaji. Ni Mungu aliyekuja miongoni mwa watu kufanya kazi Yake mwenyewe, si kutekeleza kampeni. Miongoni mwenu, hakuna hata wachache ambao wanaweza kujua kwamba kazi ya leo ni kazi ya Mungu aliye mbinguni ambaye amekuwa mwili. Siyo juu ya nyinyi kufanywa watu waliojipambanua wenye vipaji. Badala yake, ni kuwasaidia kujua umuhimu wa maisha ya binadamu, kujua hatima ya binadamu, na kuwasaidia kumjua Mungu na uzima Wake. Unapaswa kujua kwamba wewe ni uumbaji mikononi mwa Muumba. Unachopaswa kufahamu, unachopaswa kufanya, na unavyopaswa kumfuata Mungu—je, huu si ni ukweli unaopaswa kuuelewa? Je, haya si ni maono ambayo unapaswa kuyaona?
Wakati ambapo mtu ana maono ana msingi. Unapotenda kwa msingi wa kanuni hii, itakuwa rahisi zaidi kuingia ndani. Kwa njia hii hutakuwa na wasiwasi juu ya msingi wa kuingia ndani, na itakuwa rahisi sana kwako kuingia ndani. Kipengele hiki cha kuyaelewa maono, cha kuielewa kazi ni muhimu. Lazima muwe mmejiandaa na kipengele hiki. Kama hujajiandaa na kipengele hiki cha ukweli, na wewe huongea tu juu ya njia za matendo, hii ni kasoro kubwa. Nimegundua kwamba wengi wenu hamsisitizi kipengele hiki, na wakati unaposikiliza kipengele hiki cha ukweli ni kama tu kusikiliza maneno ya mafundisho. Siku moja huenda ukapoteza. Kuna baadhi ya maneno sasa ambayo huyafahamu na hujapata maarifa; kwa hiyo unapaswa kutafuta kwa uvumilivu, na siku itakuja utakapoelewa. Jiandae kidogo kidogo. Hata kama unaelewa mafundisho machache tu ya kiroho, ni bora kuliko kutoyazingatia. Ni bora kuliko kutoelewa mafundisho yoyote kamwe. Haya yote ni ya kusaidia kwa kuingia kwako, na yataondoa mashaka hayo yako. Ni bora kuliko kujazwa kwako na dhana. Ni bora zaidi kuwa na maono haya kama msingi. Bila kuwa na wasiwasi kamwe, inawezekana kuingia ndani kwa mikogo na majivuno. Kwa nini kujisumbua daima ukifuata kwa kukanganyikiwa kwa njia ya shaka? Je, hiyo si ni kama kuziba masikio yako wakati unaiba kengele? Ni jambo zuri kama nini kuingia katika ufalme kwa mikogo na majivuno! Kwa nini ujawe wasiwasi? Je, si huku hasa kungekuwa ni kupitia mateso? Unapokuwa na ufahamu wa kazi ya Yehova, wa kazi ya Yesu, na wa hatua hii ya kazi, basi utakuwa na msingi. Sasa unaweza kufikiri kwamba ni rahisi sana. Baadhi ya watu husema, “Wakati Roho Mtakatifu anapoanza kazi hii kubwa, nitakuwa na maneno yote. Ukweli kwamba kwa kweli sielewi sasa ni kwa sababu Roho Mtakatifu hajanipatia nuru sana.” Si rahisi sana; sio kwamba huko tayari kuikubali sasa, na kisha wakati utakapowadia utaitumia kwa ustadi. Si lazima iwe hivyo! Unaamini kuwa sasa umejiandaa vizuri sana, na kwamba haingekuwa shida kuwajibu wale watu wa kidini na wanadhaharia wakuu zaidi, na hata kuwakanusha. Je, ungeweza kweli kufanya hivyo? Je, ni ufahamu upi unaoweza kuuzungumzia na huo uzoefu wako duni tu? Kuwa umejiandaa na ukweli, kupigana vita ya ukweli, na kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu si kile unachofikiri ndicho–kwamba mradi Mungu yuko kazini yote yatakamilishwa. Wakati huo labda utatatizwa na swali fulani, na utafadhaishwa. Cha muhimu ni kama uko dhahiri kuhusu hatua hii ya kazi au la, na ni kiasi gani unaielewa. Ikiwa huwezi kuyashinda majeshi ya adui, na wala kuyashinda majeshi ya kidini, basi si wewe ungekuwa bure? Kama umepata uzoefu wa kazi ya leo, ukaiona kwa macho yako mwenyewe na kuisikia kwa masikio yako mwenyewe, lakini mwishowe unashindwa kushuhudia, bado unathubutu kuendelea kuishi? Ungeweza kukabiliana na nani? Usifikiri kwa kawaida sana sasa. Kazi baadaye haitakuwa rahisi kama unavyofikiri itakuwa. Kupigana vita vya ukweli si rahisi au kawaida sana. Sasa unahitaji kujiandaa. Usipokuwa umejiandaa kwa ukweli sasa, wakati utakapowadia na Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa njia ya mwujiza, basi utakuwa umechanganyikiwa.
Tanbihi:
a. Nakala ya asili inasema “Daima wewe huamini kwamba kwa kufuata unaweza kupata, kwamba kwa kuona unaweza kupata.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni