Jumamosi, 11 Novemba 2017

Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Mwenyezi Mungu alisema, Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Ijumaa, 10 Novemba 2017

Wimbo wa Injili | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Best Swahili Christian Worship Song

      
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Injili | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Best Swahili Christian Worship Song

Kama Nisingeokolewa na Mungu
Kama nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu leo,
wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu.

Alhamisi, 9 Novemba 2017

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashari,

Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

Mwenyezi Mungu alisema: Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi.

Jumatano, 8 Novemba 2017

Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

MwenyeziMungu alisema:Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Jumanne, 7 Novemba 2017

Tafuteni Maana ya Maisha - "Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi" (Video Rasmi ya Muziki)



Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi
I
Haikuwa wazi ni kwa ajili ya nani mtu anapaswa kuishi. Sasa nina jibu kwa hilo.
Nilikuwa naishi tu kwa ajili yangu mwenyewe, kutafuta hadhi tu na umaarufu.
Maombi kwa Mungu yaliyojaa maneno mema, lakini nikishikilia njia zangu mwenyewe katika maisha halisi.
Imani juu ya msingi wa kesho na majaliwa, sina ukweli au uhalisi.
Mila na sheria, zikifungia imani yangu; sikubaki na kitu ila utupu.
Kushindwa kuishi kama binadamu, sistahili upendo wa Mungu kwa ajili yangu.

Jumatatu, 6 Novemba 2017

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema: Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka.

Jumapili, 5 Novemba 2017

Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashari

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya


Mwenyezi Mungu alisema: Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaelekea kikomo, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnausubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya.

Alhamisi, 2 Novemba 2017

Tamko La Kumi Na Sita

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simmalizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wa nguvu wake, wala Siudhiki na udhaifu wake.