Jumatatu, 8 Aprili 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu 1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe 2. Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu 3. Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake
Tazama Video: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili

Jumapili, 7 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 29

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 29

Kati ya kazi inayofanywa na watu, baadhi yake hutekelezwa kwa maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu, lakini kwa sehemu yake Mungu hatoi maagizo ya wazi, ikionyesha vya kutosha kwamba kile kinachofanywa na Mungu, leo, bado hakijafichuliwa kabisa—ambalo ni kusema, mengi bado yamefichwa na bado hayajajulikana na watu.

Jumamosi, 6 Aprili 2019

Ni Nini Maana ya Krismasi, na Je, Unamwabudu Bwana Yesu Kweli?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Bwana Yesu,

Ni Nini Maana ya Krismasi, na Je, Unamwabudu Bwana Yesu Kweli?


                                             Na Siyuan
                                                 
                                           Vyanzo vya Krismasi

Kila mwaka, Krismasi inapokaribia, maduka kwenye mitaa hutayarisha maonyesho yang’aayo ya zawadi za Krismasi, pamoja na Baba Krismasi na miti ya Krismasi, na kadhalika. Kuna taa nyingi za rangi nyingi zilizoning’inizwa katika miti na kwenye majengo, na miji mizima hupambwa kwa fanusi na mapazia ya rangi nyingi, na kila mahali kuna furaha na msisimko. Kwa Ukristo, Krismasi ni likizo ya pekee sana, na miezi kadhaa kabla ya Krismasi, makanisa mengi yataanza kujishughulisha na kuandaa kila kitu kilicho muhimu kwa likizo ya Krismasi.

Ijumaa, 5 Aprili 2019

Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma


Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma

Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...), mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...), ukiangaza njia yote kwenda magharibi. Mwana wa Adamu ameshuka duniani. Mwokozi amerejea, Yeye ni Mwenyezi Mungu. Akionyesha ukweli, Ameanzisha enzi mpya. Mwana wa Adamu ameonekana. (Siyo?) Mungu amekuja. (Eh!)

Alhamisi, 4 Aprili 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 28


Sura ya 28

Mwenyezi Mungu anasema, Hali ya watu ni kwamba kadri wanavyoelewa maneno ya Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyoshuku zaidi njia ya sasa ya Mungu ya kufanya kazi. Lakini hii haina athari kwa kazi ya Mungu; maneno Yake yanapofikia kiwango fulani, kwa kawaida mioyo ya watu itabadilika. Katika maisha yao, kila mtu huyakazia macho maneno ya Mungu, na pia wao huanza kutamani sana maneno Yake—na kwa sababu ya mfichuo wa Mungu wa siku zote, wanaanza kujidharau.

Jumatano, 3 Aprili 2019

“Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”

Matamshi ya Mungu | “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atamjua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutastahili kuingia lango la ufalme wa mbinguni, maana wewe ni kikaragosi na mfungwa wa historia.

Jumanne, 2 Aprili 2019

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,
Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Xiaoxue, Malesia
      
Siku moja baada ya mlo mkuu wa siku, nilimfundisha mwanangu mvulana mkubwa jinsi ya kusoma Kichina—maneno rahisi tu, “Mbinguni, dunia, watu, na, dunia, baba, mama….” Nilimfundisha mara chache hasa, lakini bado hakuweza kuandika. Angeandika neno la kwanza na kisha kusahau lililofuata. Hasira ndani yangu ilipanda, na kunyakua rula iliyokuwa juu ya meza na kumgonga mara kadhaa. Nilimpigia kelele kwa sauti kubwa: “Wewe ni mpumbavu jinsi gani! Huwezi hata kujifunza maneno haya machache!” Mwanangu mkubwa alipigwa mpaka akalia, “waa, waa” na kutoroka na kukimbia kusimama pembeni.

Jumatatu, 1 Aprili 2019

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia, mchangamfu na mwenye nguvu za ujana, wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni. Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu. Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake. Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda. Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku, tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza.