Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Jumapili, 31 Desemba 2017
Jumamosi, 30 Desemba 2017
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Tano)
Mwenyezi Mungu anasema, Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.
9. Bwana Yesu Atenda Miujiza
1) Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo.
Ijumaa, 29 Desemba 2017
Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video
Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video
Kama Nisingeokolewa na Mungu
Kama nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu leo,
wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu.
Alhamisi, 28 Desemba 2017
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Nne)
![]() |
| Kanisa la Mwenyezi Mungu |
Mwenyezi Mungu anasema, Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na mfalme wa ibilisi, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi.
Jumatano, 27 Desemba 2017
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Tatu)
Mwenyezi Mungu anasema, Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.
Jumanne, 26 Desemba 2017
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Pili)
Mwenyezi Mungu anasema, Kama hii ilikuwa habari ya shangwe au ya kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana.
Jumatatu, 25 Desemba 2017
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III (Sehemu ya Kwanza)
Mwenyezi Mungu anasema,Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa.
Jumapili, 24 Desemba 2017
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufalme wa Milenia Umewasili
Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





