Jumanne, 30 Aprili 2019

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu.

Jumatatu, 29 Aprili 2019

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi.

Jumapili, 28 Aprili 2019

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ukweli,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane kuhusu mada ya kumfuata Mungu.

Ijumaa, 26 Aprili 2019

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, huruma,
Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. Katika kipindi hiki cha muda, hakuwahi kupata kumjua Yesu, lakini alikuwa radhi kumfuata kutokana na kuvutiwa na Yeye tu.

Alhamisi, 25 Aprili 2019

Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mimi Naeneza kazi Yangu katika nchi za Mataifa. Utukufu Wangu unamulika kotekote ulimwenguni; mapenzi Yangu yamo katika wanadamu yakitawanyika hapa na pale, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi ambayo Nimewapa. Kuanzia wakati huu kuendelea, Nimeingia katika enzi mpya, kuwaleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Niliporudi katika “nchi Yangu,” Nilianza sehemu nyingine tena ya kazi katika mpango Wangu wa asili, ili mwanadamu aje kunijua zaidi. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, kwa hiyo Naharakisha mbele na nyuma kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu.

Jumatano, 24 Aprili 2019

Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu amewaamulia kabla watu wengi kumhudumia, wakiwemo watu kutoka kila tabaka la maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni inatimia kwa urahisi. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia. Kila mtu anayemhudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na kudura ya Mungu, na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.

Jumanne, 23 Aprili 2019

Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa sababu ya hili, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani.