Ijumaa, 31 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Lazima muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kuweza kula na kunywa maneno ya Mungu ninyi wenyewe, kupitia maneno ya Mungu ninyi wenyewe, na kuishi maisha ya kiroho ya kawaida bila uongozi wa wengine; lazima muweze kuyategemea maneno ya Mungu ya leo ili kuishi, kuingia katika uzoefu wa kweli, na kuona kwa hakika. Ni wakati huo tu ndipo mtaweza kusimama imara. Leo, watu wengi hawaelewi kikamilifu majonzi na majaribio ya siku za usoni. Katika siku za usoni, watu wengine watapitia majonzi, na wengine watapitia adhabu. Adhabu hii itakuwa kali zaidi; itakuwa ni kuwasili kwa ukweli.

Alhamisi, 30 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli.

Jumatano, 29 Mei 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (1)

Neno la Mwenyezi Mungu | Utendaji (1)

Mbeleni, kulikuwa na kupotoka kwingi katika jinsi watu walipata uzoefu, na kungeweza hata kuwa kwa ajabu. Kwa sababu tu hawakuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, kulikuwa na maeneo mengi ambayo uzoefu wa watu ulienda kombo. Sharti la Mungu kwa mtu ni kwao kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Njia za mtu wa kisasa kuhusiana na chakula na mavazi, kwa mfano. Wanaweza kuvaa suti na tai na wanaweza kujifunza kiasi kuhusu sanaa ya kisasa, na katika muda wao wa ziada wanaweza kuwa na kiasi fulani cha fasihi na maisha ya burudani.

Jumanne, 28 Mei 2019

Unapaswa Kudumisha Ibada Yako Kwa Mungu

Roho Mtakatifu Anafanya kazi vipi katika kanisa sasa? Je, una ufahamu wa hilo? Ni matatizo gani makubwa zaidi yanayowakumba ndugu na dada? Wamepungukiwa na nini zaidi? Kwa sasa, kuna watu ambao wako hasi katikati ya majaribio, na wengine wao hata wanalalamika, na wengine hawasongi mbele tena kwa sababu Mungu Hazungumzi tena. Watu hawajaingia njia sahihi ya imani katika Mungu. Hawawezi kuishi wakijitegemea, na hawezi kudumisha maisha yao ya kiroho.

Jumatatu, 27 Mei 2019

Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli Katika Vitendo

Wale miongoni mwa ndugu ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi sio tu kwamba hawatashindwa kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomwasi Mungu.

Jumapili, 26 Mei 2019

Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji

Kama unamwamini Mungu, ni lazima umtii Mungu, uweke ukweli katika vitendo na utimize wajibu wako wote. Zaidi ya hayo, ni lazima uelewe mambo unayopaswa kupitia. Ikiwa unapitia tu kushughulikiwa, kufundishwa nidhamu na hukumu, kama wewe unaweza tu kumfurahia Mungu, lakini huwezi kuhisi wakati Mungu anakufundisha nidhamu au kukushughulikia, hili halikubaliki. Labda katika wakati huu wa usafishaji unaweza kushikilia msimamo wako. Hii bado haitoshi; ni lazima uendelee mbele. Funzo la kumpenda Mungu halina mwisho, na hakuna kamwe kikomo kwake.

Jumamosi, 25 Mei 2019

Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake

Kundi la watu ambao Mungu anataka kupata sasa ni wale ambao wanajitahidi kushirikiana na Mungu, wanaoweza kuiheshimu kazi Yake, na wanaoamini kuwa maneno Anayonena Mungu ni ya kweli, wale wanaoweza kuweka mahitaji ya Mungu katika vitendo. Ni wale walio na uelewa wa kweli katika mioyo yao. Ni hao ndio wanaoweza kukamilishwa, na wale ambao bila shaka watatembea katika njia ya ukamilisho. Wale wasio na uelewa wa wazi wa kazi ya Mungu, wale wasiokula na kunywa neno la Mungu, wale wasiotilia maanani neno la Mungu, na wale wasio na upendo wowote kwa Mungu katika mioyo yao—watu kama hao hawawezi kufanywa wakamilifu.

Ijumaa, 24 Mei 2019

Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu

Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:
1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.
2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.

Alhamisi, 23 Mei 2019

Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Njia ambayo Roho Mtakatifu huchukua ndani ya watu ni kuvuta kwanza mioyo yao kutoka kwa watu, matukio, na vitu vyote, na kuingiza ndani ya maneno ya Mungu ili ndani ya mioyo yao wote waamini kwamba maneno ya Mungu hayana shaka kabisa na ni kweli kabisa. Kwa vile unaamini katika Mungu lazima uamini katika maneno Yake; ikiwa umeamini katika Mungu kwa miaka mingi lakini hujui njia ambayo Roho Mtakatifu hufuata, wewe kweli ni muumini? Ili kutimiza maisha ya mtu wa kawaida na maisha yanayofaa ya mtu na Mungu, lazima kwanza uamini maneno Yake. Ikiwa hujakamilisha hatua ya kwanza ya kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya ndani ya watu, huna msingi.

Jumatano, 22 Mei 2019

Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake.

Jumanne, 21 Mei 2019

Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi

Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kiwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi. Mambo si rahisi kama ulivyofikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hapo ndipo unapoumiliki uhalisi, hapo ndipo umeupata uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu.

Jumatatu, 20 Mei 2019

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Katika matendo, amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye.  Kuzishika amri na kuutenda ukweli;vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana.

Jumapili, 19 Mei 2019

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

Hapo awali sana, umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa ulitajwa katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni kile kitu kimoja tu cha zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa sahihi kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa chakula na vinywaji vinaweza kuwa vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hapajakuwa na mabadiliko makubwa katika hali kanisani. Imekuwa kama kuweka divai ya kale katika kiriba kipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika kabisa.

Jumamosi, 18 Mei 2019

Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua.

Ijumaa, 17 Mei 2019

Jinsi ya Kuingia Ndani ya Hali ya Kawaida

Watu wanapozidi kuwa wapokelevu wa maneno ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kupata nuru na wanaendelea zaidi kufuatilia maarifa ya Mungu kwa njaa na kiu ya hali ya kuwa mwenye haki. Ni wale tu ambao wanapokea maneno ya Mungu wanaweza kuwa na matukio ya undani zaidi na yenye utajiri zaidi; ni wale tu ambao maisha yao yanakuwa ya kupendeza zaidi na zaidi. Kila mtu ambaye anafuatilia uzima lazima ashughulikie haya kana kwamba ni kazi yake, na ni sharti awe na hisia kuwa hawezi kuishi bila Mungu, na hakuna mafanikio yoyote bila Mungu, na kila kitu ni ubatili bila Mungu. Wanapaswa kuwa na azimio la kutofanya lolote bila uwepo wa Roho Mtakatifu, na kutotaka kutenda lolote zaidi kama matendo yao hayazai matunda.

Alhamisi, 16 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neno la Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (7)

Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii. Hivyo, imetayarishiwa hasa sisi, na haijalishi ikiwa tutapokea baraka au kupata taabu, hakuna mwingine anayeweza kutembea njia hii.

Jumatano, 15 Mei 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu swahili worship songs | Njia Yote Pamoja na Wewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neema,

  • I
  • Nilikuwa kama mashua,
  • ikielea baharini.
  • Ulinichagua,
  • na mahali pazuri Uliniongoza.
  • Sasa katika familia Yako,
  • nikipewa joto na upendo Wako,
  • nina amani kabisa.

Jumanne, 14 Mei 2019

Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili


Neno la Mungu | “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” Sehemu ya Pili


Mwenyezi Mungu anasema, “Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumatatu, 13 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (6)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (6)

Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake. Kwa hiyo mpaka leo Sijaweza kuueleza kwa dhahiri—ni kama kwamba ni kitendawili kisichofumbuliwa. Lakini kwa jumla, kundi hili letu limejaaliwa na Mungu, na Ninaendelea kuamini kwamba Mungu ana kazi nyingine ndani yetu.

Jumapili, 12 Mei 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu

Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.
Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.
Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.
Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.
Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.
Tunatafakari, kufikiri maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu anatuangazia.

Jumamosi, 11 Mei 2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu. Ilhali tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ijumaa, 10 Mei 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu.

Alhamisi, 9 Mei 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake.”

Yaliyopendekezwa: “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 8 Mei 2019

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha. Hakuna mtu anayejali ni kwa nini leo Mungu amewachagua tu—kikundi kisichostahili mno—kukifanyia kazi, hivyo je, kazi hii inafanywa vibaya? Je, hii ni kazi ya uangalizi wa muda mfupi?

Jumanne, 7 Mei 2019

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neno la Mungu,

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

Jumatatu, 6 Mei 2019

Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Yudea. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyoondoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Waisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Waisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Yudea, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Waisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote.

Jumapili, 5 Mei 2019

Inapokuja kwa Mungu, Ufahamu Wako Ni Upi?

Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno hili “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa.

Jumamosi, 4 Mei 2019

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewazia hili: Mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.

Ijumaa, 3 Mei 2019

Matamshi ya Kristo | Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hujitahidi kupata mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii hasa, wengi kati yenu wanajaribu daima kujipendekeza kwa Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu aliye ndani ya mioyo yenu.

Alhamisi, 2 Mei 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa
Yaliyopendekezwa: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"
Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumatano, 1 Mei 2019

Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii

1. Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupaswi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.
3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu.