Jumanne, 17 Julai 2018

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, kanisa, injili,
Imani katika Mungu
Utambulisho 
Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika. Huko, mjadala ulijitokeza miongoni mwa Zheng Xun na wafanyakazi wenzake kuhusu kama muumini katika Mungu anapaswa kutii wale walio madarakani au la. Yu Congguang alitoa ushirika kwa kuzingatia suala hili na kuondoa kuchanganyikiwa kwao. Ushirika wa Yu Congguang ulikuwa wa manufaa sana kwao, na wote wakaanza kutafuta na kujifunza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Jumatatu, 16 Julai 2018

Vita Baina ya Haki na Uovu | Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, maafa, wokovu,

Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

Fang Xin, Beijing
Agosti 15, mwaka wa 2012
Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia. Kila wakati ninapowaza kuhusu ukweli kwamba binti yangu tayari ana umri wa miaka thelathini, na angali bado hajapata mwenzi wa kufaa, mimi hulalamika kwa Mungu; mwanangu wa kiume hujali tu kuhusu kujifurahisha, na licha ya kutokuwa na mapato yoyote, yeye hutumia pesa kwa ubadhirifu, kwa hiyo mimi hulalamika; na mme wangu mzee huenda kazini, lakini msimamizi wake huwa hamlipi–na mimi hulalamika kuhusu hili pia .... Mimi hulalamika kwa pande zote, na mara nyingi humwelewa Mungu visivyo.

Jumapili, 15 Julai 2018

Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo - Sura ya 45. Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa

Imesemwa “Yeye afuataye hadi mwisho ataokolewa,” lakini hili ni rahisi kuweka katika vitendo? Sio, na watu wengine hawawezi kufuata hadi mwisho. Pengine watakapokabiliwa na wakati wa majaribu, ama uchungu, ama jaribio, basi wanaweza kuanguka, na kutoweza kusonga mbele tena. Mambo ambayo hufanyika kila siku, yawe ni makubwa ama madogo, yanaweza kutikisa uthabiti wako, kuumiliki moyo wako, kuzuilia uwezo wako wa kufanya jukumu lako, ama kudhibiti kuendelea kwako mbele—vitu hivi vyote vinahitaji kuchukuliwa kwa uzito, lazima vichunguzwe kwa makini ili kuutafuta ukweli, na ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu.

Jumamosi, 14 Julai 2018

Vita Baina ya Haki na Uovu | Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

maafa, Mafuriko,
Bila Ya Wokovu wa Mungu, Singeweza Kuwa Hapa Leo

Zhang Jin, Beijing
Agosti 16, 2012
Mimi ni dada mzee mwenye miguu miwili yenye kasoro. Hata wakati hali ya hewa ni nzuri nje, nina shida kutembea, lakini wakati maji ya mafuriko yalipokuwa karibu kunimeza, Mungu aliniruhusu kutoroka hatari kimiujiza.
Ilikuwa Julai 21, mwaka wa 2012. Siku hiyo mvua ya mfoko ilinyesha, na nilikuwa tu nje nikitimiza wajibu wangu. Baada ya saa 10:00 mchana, mvua ilikuwa bado haijaisha.

Ijumaa, 13 Julai 2018

Ni tofauti gani halisi zilizopo kati ya Mungu mwenye mwili na watu wanaotumiwa na Mungu❓

📜"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (Mathayo 3:11).
📚"Na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

Alhamisi, 12 Julai 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ubia wa Kweli

Fang Li    Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan
Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujadili kitu chochote, wakati mwingine hata nikamwomba aonyeshe dosari zangu, na hatukupigana kamwe, hivyo nilidhani tulikuwa tumefanikisha ubia wenye kuridhisha. Lakini kama ukweli ulivyofichua, ubia wenye kuridhisha kwa kweli haukuwa kama kitu chochote nilichosadiki.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,

Jumatano, 11 Julai 2018

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili,

Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Ndugu wawili wa kawaida, Beijing
Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.
Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja. Muda mfupi baada ya saa 4 jioni, nilitoka nje mtaani ili kuangalia na nikaona kuwa maji yalikuwa kila mahali.

Jumanne, 10 Julai 2018

Sura ya 1 Lazima Ujue Kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Mbingu na Dunia na Kila kitu Ndani Yao

2. Mwenyezi Mungu Ndiye Yesu Aliyerudi.

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua.