Ijumaa, 8 Februari 2019

4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Yesu

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu angeshikilia ukweli kwamba "Yehova ni Mungu" na "Yesu ni Kristo," ukweli ambao unazingatiwa kwa kipindi kimoja, basi mwanadamu hataweza kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu.

Alhamisi, 7 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 15

Sura ya 15

Mwenyezi Mungu alisema, Tofauti kubwa zaidi kati ya Mungu na mwanadamu ni kwamba kila mara maneno ya Mungu hugonga ndipo, na hakuna kilichofichwa. Kwa hiyo hali hii ya tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika maneno ya kwanza ya leo. Kipengele kimoja ni kuwa yanaonyesha tabia halisi ya mwanadamu, na kipengele kingine ni kuwa yanafichua wazi tabia ya Mungu. Hizi ni asili kadhaa za jinsi maneno ya Mungu yanaweza kutimiza matokeo. Hata hivyo, watu hawalielewi hili, kila mara wao huja kujijua tu katika maneno ya Mungu lakini "hawajamchangua" Mungu.

Jumatano, 6 Februari 2019

Swahili Christian Music Video | "Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu" | God Led Me Onto the Right Path of Life

I
Kwa ajili ya faida niliacha viwango vyote vya mwenendo,
na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.
Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.
Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.
Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,
bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Jumanne, 5 Februari 2019

3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

Maneno Husika ya Mungu:
Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita?

Jumatatu, 4 Februari 2019

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 14

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 14

Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu hajawahi kamwe kujifunza chochote kutoka kwa neno la Mungu. Badala yake, mwanadamu huthamini tu umbo la nje la neno la Mungu, lakini kutojua maana yake halisi. Kwa hivyo, ingawa wengi wa watu wanapenda neno la Mungu, Mungu asema kwamba hawalithamini kwa kweli. Hili ni kwa sababu katika maoni ya Mungu, hata ingawa neno Lake ni kitu cha thamani, watu hawajaonja utamu wake halisi.

Jumapili, 3 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Saba"

Mwenyezi Mungu anasema, "Nyie watu Wangu, myasikiapo maneno Yangu, je mnaielewa nia Yangu? Mnaiona roho Yangu? Mlipoipitia njia ya huduma hapo awali mlikumbana na panda-shuka, maendeleo mazuri na vikwazo, na zilikuwepo nyakati mlipokuwa katika hatari ya kuanguka na hata kunisaliti Mimi; lakini mlifahamu kuwa Nilikuwa katika harakati za kuwakomboa kila wakati? Kwamba kila wakati Nilikuwa napaza sauti Yangu kuwaita na kuwakomboa?

Jumamosi, 2 Februari 2019

1. Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

1. Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu" (LAW. 11:45).
"Na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana" (EBR. 12:14).
"Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho" (YN. 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako.

Ijumaa, 1 Februari 2019

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova" (ISA 2:2-5).