Jumamosi, 12 Oktoba 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”


Mwenyezi Mungu anasema, “Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.”

Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu


Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. 

Jumatano, 9 Oktoba 2019

Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

Mo Zhijian Mkoa wa Guangdong

Nilizaliwa katika eneo maskini, la mbali lenye milima ambako tumefukiza na kumwabudu Budha kwa vizazi vingi. Kuna hekalu za Budha sehemu hiyo kote ambako familia zote zingekwenda kuchoma uvumba; hakuna mtu yeyote aliyewahi kumwamini Mungu kamwe. Katika mwaka wa 1995, mimi na mke wangu tulikuwa katika sehemu nyingine ya nchi ambapo tulimwamini Bwana Yesu; baada ya sisi kurudi tulianza kushiriki injili na idadi ya watu ambao waliikubali ilikua polepole hadi watu zaidi ya 100. Kwa sababu watu zaidi na zaidi walikuwa wakimwamini Mungu, liliishtua serikali ya mitaa. Siku moja mwaka wa 1997, polisi waliniita kwenda kituo cha polisi cha mahali palepale, ambapo mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Umma ya Wilaya, Mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Taifa, mkuu wa Ofisi ya Dini na mkuu wa kituo cha polisi na vilevile maafisa wachache wa polisi walikuwa wananisubiri. 

Jumatano, 25 Septemba 2019

"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 1 Matukio ya Kuzimu | Kwaya za Injili


"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 1 Matukio ya Kuzimu | Kwaya za Injili


Je, unafikiria kuna kuzimu? Je, kuzimu iko namna gani hasa? Tafadhali fuatilia dondoo hii ya video!

Jumanne, 24 Septemba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)

Maneno ya Mungu, neno la Mungu, siku za mwisho

Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani.

Jumatatu, 23 Septemba 2019

maneno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni.

Jumapili, 22 Septemba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (2)


Kazi na kuingia kwenu ni duni kabisa; mwanadamu hafikirii kwamba kazi ni muhimu na hata yeye ni mzembe zaidi na kuingia. Mwanadamu haoni haya kuwa mafunzo mazuri anayopaswa kuingia ndani; kwa hivyo, katika uzoefu wake wa kiroho, kwa kweli yote ambayo mwanadamu huona ni njozi. Si mengi yanatakiwa kutoka kwenu kuhusu uzoefu wenu katika kazi, lakini, kama yule anayetakiwa kukamilishwa na Mungu, mnapaswa kujifunza kumfanyia Mungu kazi ili hivi punde muweze kuupendeza moyo wa Mungu. Kotekote katika enzi, wale waliofanya kazi wameitwa wafanyakazi au mitume, ambayo inahusu idadi ndogo ya watu waliotumiwa na Mungu.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)

Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu.