Jumatano, 31 Oktoba 2018

Sura ya 5 Lazima Uujue Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili.

Jumanne, 30 Oktoba 2018

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi | Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu Lina Malengo Yapi?

Kanisa la Mwenyezi Mungu hunyunyizia na kuwaongoza waumini wake kwa mujibu kamili wa maneno ya Mungu katika Biblia na Neno Laonekana Katika Mwili yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ili kwamba kila muumini anaweza, chini ya uongozi, utolewaji, unyunyiziwaji, na uongozwaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, kuelewa ukweli wote katika maneno ya Mungu, kumiliki mtazamo sahihi juu ya maisha na maadili, kuwa na malengo sahihi ya kufuatilia, kufuata njia ya Mungu, kushikilia maagizo ya Mungu, kumtukuza Mungu kwa kuwa nuru na chumvi ya dunia, na kusifiwa na Mungu, na kuwa na sifa kamili kurithi ahadi za Mungu.

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi | Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu huamini katika Mungu huyo huyo. Watu wanaoelewa historia ya dini wanajua kwamba Uyahudi wa Israeli ulizaliwa na kazi ambayo Yehova Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria. Ukristo, Ukatoliki, na Othodoksi ya Mashariki yote yalikuwa makanisa yaliyoibuka baada ya Bwana Yesu mwenye mwili kufanya kazi ya ukombozi. Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwepo wakati Mungu alipopata mwili wakati wa siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu.

Jumapili, 28 Oktoba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 35

Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kwa bako.” Hii ni kweli kabisa, lakini watu bado hawawezi kulielewa kabisa wazo hili. Kutokana na hili, sehemu ya kazi ambayo wamefanya imekuwa si lazima. Mungu alisema, “Mimi husaidia na kuwaruzuku kwa mujibu wa kimo chao.

Jumamosi, 27 Oktoba 2018

Wimbo wa Injili | Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa | Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu

Wimbo wa Injili | Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa | Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu

I
Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu,
Amekuwa akifichua kwao
Kiini Chake na vile Alivyo na Alicho nacho, bila kukoma, kila wakati.
Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,
Mungu huzungumza na kufanya kazi ili kuonyesha tabia Yake na kiini.
Havijawahi kufunikwa wala kufichwa kamwe, vimeachiliwa bila kusita,
Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,
vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda - Kuahidi Maisha Yangu kwa Moyo wa Ibada

Zhou Xuan Mkoa wa Shandong
Mnamo Aprili 3, mwaka wa 2003, niliambatana na dada mmoja kumtembelea muumini mpya. Muumini huyu mpya alikuwa bado hajawekwa katika ukweli na aliishia kuturipoti. Kwa sababu hiyo, askari wanne waovu wenye nguo za raia walikuja na kwa ugomvi kutuingiza sisi wawili katika gari lao na kutupeleka kwa kituo cha polisi. Njiani, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi mno, kwa sababu mwilini mwangu nilikuwa na peja ya mawasiliano, orodha isiyo kamili ya majina ya wanajumuiya wa kanisa letu, na daftari dogo.

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova.

Jumatano, 24 Oktoba 2018

Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?

Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. … Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria.”