Alhamisi, 28 Februari 2019

Muziki wa Injili "Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele"

Muziki wa Injili "Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele"

Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake yanaamuliwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali au kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni anayapokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.
Maneno ya Mungu ni ukweli, usiobadilika milele.
Mungu ndiye mpaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.

Jumatano, 27 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku”

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuanzia leo, Mungu ataweza kuwafanya watu wasiokuwa na fikira za kidini kuwa watimilifu kwa njia rasmi, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu, pamoja na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo na hekima nyingi na isiyoisha. Kazi yake ya kustaajabisha na matamshi yake yenye thamani ni vitu ambavyo vipo ili watu wengi zaidi kuweza kufurahia.

Jumanne, 26 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu.”

Jumatatu, 25 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 17

Sura ya 17

Mwenyezi Mungu alisema: Kwa kweli, maneno yote kutoka katika kinywa cha Mungu ni mambo ambayo wanadamu hawayajui; yote ni lugha ambayo watu hawajasikia, kwa hiyo inaweza kusemwa hivi: Maneno ya Mungu yenyewe ni siri. Watu wengi kwa kutojua wanaamini kwamba ni mambo tu ambayo watu hawawezi kutimiza kimawazo, mambo ya mbinguni ambayo Mungu anawawezesha watu kuyajua sasa, au ukweli kuhusu kile Mungu anachofanya katika ulimwengu wa kiroho ni siri.

Jumapili, 24 Februari 2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP. Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa.

Jumamosi, 23 Februari 2019

Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu, Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe ilhali hawawezi kufanya kazi ya Mungu ni wadanganyifu.
Wanaojifanya kuwa Kristo hatimaye wataanguka,
ingawaje wanadai kuwa Kristo,
hawana kiini chochote cha Kristo.

Ijumaa, 22 Februari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu. Maono kama hayo pia ni usimamizi wa Mungu, na kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu. Mahitaji ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa mwanadamu wakati wa kazi Yake, wakati uo huo, yanaitwa “vitendo” vya mwanadamu.

Alhamisi, 21 Februari 2019

Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima | Sura ya 16

Sura ya 16

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa watu, Mungu ni mkuu mno, mwenye utele mno, wa ajabu mno, Asiyeeleweka mno; machoni pao, maneno ya Mungu hupaa juu, na huonekana kama kazi bora sana ya ulimwengu. Lakini kwa vile watu wana kasoro nyingi sana, na akili zao ni za kawaida sana, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa uwezo wao wa kukubali ni haba mno, bila kujali vile Mungu hunena maneno Yake kwa dhahiri, wanabaki palepale bila kutikisika, kana kwamba wana ugonjwa wa akili.