Jumamosi, 31 Machi 2018

Kuhusu Biblia (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

Kuhusu Biblia (2)

Mwenyezi Mungu alisema, Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, mnajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika Agano la Kale linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao.

Ijumaa, 30 Machi 2018

Kuhusu Biblia (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

Kuhusu Biblia (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Biblia inapaswa kuangaliwaje kuhusiana na imani kwa Mungu? Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini tunawasiliana swali hili? Kwa sababu wakati ujao utaeneza injili na kupanua kazi ya Enzi ya Ufalme, na haitoshi tu kuweza kuzungumza juu ya kazi ya Mungu leo. Ili kupanua kazi Yake, ni muhimu zaidi kwamba unakuwa na uwezo wa kubadilisha dhana za watu za dini ya kale na njia za kale za imani, na kuwaacha wakiwa wameshawishika kabisa—na kufikia katika hoja hiyo Biblia inahusishwa.

Alhamisi, 29 Machi 2018

Yote kuhusu Mjadala wa "Iwapo Biblia Inatiwa Msukumo na Mungu"


Yote kuhusu Mjadala wa "Iwapo Biblia Inatiwa Msukumo na Mungu"

   Kwa miaka elfu mbili, dunia ya kidini imetegemea kile alichosema Paulo kuhusu Biblia kutiwa msukumo na Mungu na daima iliamini kwamba “Biblia ni maneno ya Mungu,” na “Biblia inamwakilisha Bwana.” Je, mawazo haya ni sahihi? Video hii itafichua majibu kwako!

Jumatano, 28 Machi 2018

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo.

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati.

Jumanne, 27 Machi 2018

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa na Yohana ilisikika kotekote katika nchi, hivyo ilienea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa Uyahudi, na kila mtu alimwita nabii.

Jumatatu, 26 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni


Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni
Watu wengine huamini, kwa kuwa Mungu aliweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno moja, kuweza kuwafufua wafu kwa neno moja, Mungu pia Ataweza kubadili taswira zetu mara moja, kutufanya watakatifu, kutuinua hewani kukutana na Bwana wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Je, kweli ni ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Je, kazi ya kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho rahisi hivyo jinsi tunavyofikiri? Mungu husema, "Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo zaidi.

Jumapili, 25 Machi 2018

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu,

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Mwenyezi Mungu alisema, Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Mwenyezi Mungu alisema, Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake.

Jumamosi, 24 Machi 2018

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu, Kristo,

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni


Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

Ijumaa, 23 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?

Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?

     Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja.

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu.

Alhamisi, 22 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V | Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Tano)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
E. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
(Sehemu ya Tano)

E. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, mienendo ya kijamii ni kitu kipya? (La.) Hivyo ilianza lini? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi?

Jumatano, 21 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V | Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Nne)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Sehemu ya Nne)

C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao.

Jumanne, 20 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V | Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Tatu)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Sehemu ya Tatu

Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V | Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,
Majaribu ya Shetani

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

(Sehemu ya Pili)

Mwenyezi Mungu alisema, Kuhusu neno “takatifu,” juujuu linaonekana rahisi sana kuelewa, siyo? Kwa kiwango cha chini kabisa watu wanaamini neno “takatifu” linamaanisha nadhifu, isiyo na doa, tukufu, na safi, kama tu katika wimbo tulioimba karibuni “Upendo Safi Bila dosari,” ambapo “takatifu” na “upendo” yamewekwa pamoja, ambayo ni sahihi; hii ni sehemu yake, upendo wa Mungu ni sehemu ya kiini Chake, lakini si kiini chote. Hata hivyo, katika mitazamo ya watu, wanaona neno na kulishirikisha na vitu ambavyo wao wenyewe wanaviona kuwa nadhifu na safi, ama na vitu ambavyo wao binafsi wanafikiri havina doa wala havina dosari.

Jumatatu, 19 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V 

(Sehemu ya Kwanza)

Utakatifu wa Mungu (II)

Habari za jioni kila mtu! (Habari ya jioni Mwenyezi Mungu!) Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
Kiitikio: “Upendo” unarejelea hisia safi bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu.

Jumapili, 18 Machi 2018

Swahili Gospel Movie "Vunja Pingu Na Ukimbie" | Bwana ni Mchungaji Wangu

Lee Chungmin alikuwa mzee wa kanisa fulani huko Seoul, Korea ya Kusini. Kwa zaidi ya miaka ishirini, alimtumikia Bwana kwa shauku kubwa, akamakinika kikamilifu juu ya kusoma Biblia. Akifuatia mfano wa viongozi wake wa kidini, alidhani kuwa kumwamini Bwana kulimaanisha kuiamini Biblia, na kwamba kuwa na imani katika Biblia kulikuwa sawa kabisa na kuwa na imani katika Bwana. Aliamini kwamba almuradi angeshika Biblia, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi zilimbana kama jozi ya pingu, zikimzuia kufuata nyayo za Mungu na kumwamini Mungu. Matokeo yake, Lee Chungmin kamwe hakufikiria kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho …

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Jumamosi, 17 Machi 2018

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

  Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu.

Ijumaa, 16 Machi 2018

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Alhamisi, 15 Machi 2018

Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"

Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"

I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili
Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,
kama tu vile jua la haki likichomoza;
mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.
Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma
Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,
Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.
Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.
Mungu uliyekuwa na kiu naye, Mungu niliyemngoja,
leo anaonekana kwetu kwa utendaji.

Jumatano, 14 Machi 2018

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu.

Jumanne, 13 Machi 2018

Utangulizi wa programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu | Injili ya kurudi kwa Bwana Yesu


Utangulizi wa programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu | Injili ya kurudi kwa Bwana Yesu

Ili kutimiza shauku kuu ya watu kutoka asili mbalimbali ya kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Kanisa la Mwenyezi Mungu limetoa programu yake ya kwanza ya simu ya mkononi. 

Jumatatu, 12 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV (Sehemu ya Tatu)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV  (Sehemu ya Tatu)

Utakatifu wa Mungu (I)

Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Mwenyezi Mungu alisema, Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu.

Jumapili, 11 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu


Kanisa la Mwenyezi MunguSwahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

Utambulisho

Fu Jinhua alikuwa mzee wa kanisa la nyumba nchini China. Kama Wakristo wengine wengi, alijitolea kwa Bwana kwa shauku kubwa, na alifanya kazi kwa bidii katika kazi yake kwa ajili Yake. Alikuwa hasa mwenye kujiamini, na alijiona kuwa mtu ambaye alimpenda Bwana kweli. Baada ya kumfuata Bwana kwa miaka mingi, aliamini kwa moyo wote kwamba Biblia ilikuwa imefunuliwa na Mungu, na kwamba maneno katika Biblia yote yalikuwa maneno ya Mungu.

Jumamosi, 10 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

(Sehemu ya Pili)

3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

Ijumaa, 9 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV (Sehemu ya Kwanza)

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema, Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa.Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde unapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia kwako kutakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kufuatilia kwako. Kwa njia hiyo, uzoefu na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi.

Alhamisi, 8 Machi 2018

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu mwenye mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na wakamsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, mwanadamu si adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa na sifa za kumshuhudia Mungu?

Jumatano, 7 Machi 2018

Ukweli Wafichuliwa Kuhusu Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 – CCP Ilikuwa Mwelekezi wa Siri wa Tendo Zim

Ukweli Wafichuliwa Kuhusu Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 – CCP Ilikuwa Mwelekezi wa Siri wa Tendo Zima

Utambulisho

Katika mwaka wa 2014, CCP ilibuni bila msingi maalum Tukio la Zhaoyuan lenye sifa mbaya la mnamo 5/28 katika jimbo la Shandong ili kutunga msingi wa maoni ya umma kwa ajili ya ukomeshaji kamili wa makanisa ya nyumba, na ikaeneza uwongo duniani kulaani na kuliharibia jina Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, baadhi ya washiriki wasiokusudiwa ambao hawakujua ukweli walidanganywa na propaganda za CCP. Katika programu hii, mashaka kadhaa makuu yanayoizunguka kesi hii yatafichuliwa ili kuchanganua uongo wa CCP mmojammoja na kukuelezea wazi ukweli, na kufichua kabisa ukweli kuhusu Tukio la Zhaoyuan la Shandong mbele ya ulimwengu.

Jumanne, 6 Machi 2018

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu.

Jumatatu, 5 Machi 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Ukamilifu wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii yamefanyika kulingana na hali za ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji.

Jumapili, 4 Machi 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III (Sehemu ya Tano)

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Mamlaka ya Mungu (Sehemu ya Tano)

Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba

Mwenyezi Mungu alisema, Awamu sita zilizofafanuliwa hapo juu ni awamu muhimu zilizowekwa wazi na Muumba ambazo kila mtu wa kawaida lazima apitie katika maisha yake. Kila mojawapo ya awamu hizi ni za kweli; hakuna mojawapo kati yazo ambayo inaweza kuepukwa, na zote zinasheheni uhusiano na kuamuliwa kabla kwa Muumba na ukuu Wake. Hivyo basi kwa binadamu, kila mojawapo ya awamu hizi ni sehemu muhimu ya kujikagua, na namna ya kupitia kila mojawapo vizuri ni suala muhimu sana ambalo nyinyi nyote mnakabiliwa nalo.

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III (Sehemu ya Nne)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,
(Sehemu ya Nne)
Kifo: Awamu ya Sita
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia.

Jumamosi, 3 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III (Sehemu ya Tatu)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,
(Sehemu ya Tatu)
Uhuru: Awamu ya Tatu
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c]lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.

Ijumaa, 2 Machi 2018

Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu


Swahili Gospel Song "Sala ya Watu wa Mungu" | Kuishi katika Upendo wa Mungu

Utambulisho

Watu wa Mungu wanainuliwa mbele ya kiti Chake cha Enzi,
maombi mengi mioyoni mwao.
Mungu huwabariki wote wanaorejea Kwake;
wote wanaishi katika mwanga.
Omba Roho Mtakatifu alipe nuru neno la Mungu
ili kwamba tujue kikamilifu mapenzi ya Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Bwana Yesu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi


Mwenyezi Mungu alisema, Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Alhamisi, 1 Machi 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi Katika Enzi ya Sheria

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi katika Enzi ya Sheria

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake.