Ijumaa, 28 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale “watoto” wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba watu hawa wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong’aa kuanzia hapo kwendelea. Wakati huo, mtaishi katika bonde la kivuli.

Alhamisi, 27 Juni 2019

Watu Wanaoweza Kuwa Watiifu Kabisa Kwa Utendaji wa Mungu Ndio Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli

Kuwa na ujuzi wa utendaji na kuwa na uwezo wa kuona wazi kazi ya Mungu—yote haya yanaonekana katika maneno Yake. Ni katika maneno ya Mungu tu ndio unaweza kupata nuru, hivyo unapaswa kujitayarisha na maneno Yake zaidi. Gawa ufahamu wako kutoka kwa maneno ya Mungu katika ushirika, na kupitia katika ushirika wako wengine wanaweza kupata nuru na unaweza kuwaongoza watu kwenye njia—njia hii ni ya utendaji. Kabla ya Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili yenu, kila mmoja wenu lazima kwanza ajitayarishe na maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kufanya—ni kipaumbele cha haraka.

Jumatano, 26 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (6)

Leo, watu wengi hawana hata urazini au kujitambua kwa Paulo, ambaye, ingawa aliangushwa na Bwana Yesu, tayari alikuwa na azimio la kufanya kazi na kuteseka kwa ajili Yake. Yesu alimpa ugonjwa, na baadaye, Paulo aliendelea kuvumilia ugonjwa huu mara alipoanza kufanya kazi. Kwa nini alisema alikuwa na mwiba mwilini mwake? Mwiba, kwa kweli, ulikuwa ugonjwa, na kwa Paulo, ulikuwa ugonjwa wa kufisha. Haijalishi alivyofanya kazi vizuri au jinsi azimio lake kuteseka lilivyokuwa kuu, alikuwa na ugonjwa huu kila mara. Paulo alikuwa mwenye uhodari thabiti zaidi kuliko ninyi watu wa leo; hakuwa tu mwenye uhodari mzuri, lakini pia alikuwa na kujitambua na alikuwa na urazini zaidi kuwaliko ninyi.

Jumanne, 25 Juni 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Uzoefu

Katika uzoefu wote wa Petro, alikumbana na mamia ya majaribio. Ingawa watu wa leo wanafahamu neno “jaribio,” wao huchanganyikiwa kuhusiana na maana yake ya kweli na hali. Mungu hutuliza azimio la watu, husafisha imani yao, na hukamilisha kila sehemu yao—na hii hufanikishwa kimsingi kupitia majaribio, ambayo pia ni kazi ya Roho Mtakatifu iliyofichwa. Inaonekana kama kwamba Mungu amewaacha watu, na kwa hivyo wasipokuwa waangalifu, watayaona majaribio haya kama majaribu ya Shetani. Kwa kweli, majaribio mengi yanaweza kufikiriwa kuwa majaribu, na hii ni kanuni na sheria ambazo Mungu hufanya kazi kupitia kwazo.

Jumatatu, 24 Juni 2019

Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wa watu unaegemea upande mmoja sana. Bila kufahamu hali nyingi kwa kweli, huwezi kufikia mbadiliko katika tabia yako. Ikiwa umeelewa hali nyingi, basi utaweza kuelewa maonyesho mbalimbali ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuona wazi na kutambua mengi ya kazi ya pepo wabaya.

Jumapili, 23 Juni 2019

Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Ushuhuda wa Maisha, Wakristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu

Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnampa Mungu nguvu zenu zote na kujitoa kwa ajili Yake, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu.

Jumamosi, 22 Juni 2019

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu yake muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kiasi, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na kusikiza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na ukiendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kukamilishwa. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kiasi fulani cha kazi ya Mungu, alipata umaizi kiasi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia.

Ijumaa, 21 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (5)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (5)

Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu alizungumza maneno kiasi na Akatekeleza hatua moja ya kazi. Kulikuwa na muktadha kwayo, na yalikuwa ya kufaa kwa hali za watu kwa wakati huo; Yesu alinena na kufanya kazi kama ilivyostahili muktadha wa wakati huo. Pia Alinena unabii kiasi. Alitabiri kwamba Roho wa ukweli angekuja wakati wa siku za mwisho, wakati ambapo Roho wa ukweli angetekeleza hatua ya kazi. Ambalo ni kusema, nje ya kazi ambayo Yeye Mwenyewe alikuwa Afanye wakati wa enzi hiyo, Hakuwa dhahiri kuhusu lingine lolote; yaani, kulikuwa na mipaka kwa kazi iliyoletwa na Mungu mwenye mwili. Hivyo, Alifanya tu kazi ya enzi hiyo, na hakufanya kazi nyingine ambayo haikuwa na uhusiano na Yeye.

Alhamisi, 20 Juni 2019

Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu

Agano Jipya la Biblia lina nyaraka kumi na tatu za Paulo. Barua hizi kumi na tatu ziliandikwa na Paulo kwa makanisa yaliyomwamini Yesu Kristo wakati wa kazi yake. Yaani, aliziandika barua baada ya Yesu kupaa mbinguni na alifufuliwa. Barua zake ni ushuhuda wa ufufuo wa Bwana Yesu na kupaa mbinguni baada ya kifo Chake, na zinahubiri njia ya watu kutubu na kuubeba msalaba. Kwa kweli, njia hizi na shuhuda zote zilikuwa za kuwafundisha ndugu na dada katika sehemu mbalimbali za Uyahudi wakati huo, kwa sababu wakati huo Paulo alikuwa mtumishi wa Bwana Yesu, na alikuwa ameinuliwa kutoa ushuhuda kwa Bwana Yesu.

Jumatano, 19 Juni 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliumba vitu vyote kuhusiana, kupatana na kutegemeana. Alitumia njia hii na kanuni hizi kudumisha kuendelea kuishi na uwepo wa vitu vyote na kwa njia hii binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili.

Jumanne, 18 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” I Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Kwanza
Mwenyezi Mungu anasema, “Tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichwa, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne


Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani.

Jumapili, 16 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu.

Jumamosi, 15 Juni 2019

Je, Wale Wasiojifunza na Wasiojua Chochote si Wanyama tu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Ni mbinu gani iliyo ya kufaa zaidi ya ufukuziaji katika njia ya leo? Ni umbo la aina gani unalopaswa kujiona mwenyewe kama katika ufukuziaji wako? Unapaswa kujua namna ya kushughulikia kila kitu kinachokufika wewe sasa, yawe ni majaribio au mateso, kuadibu bila huruma au laana—unapaswa kufikiria kwa makini haya yote. Mbona Nasema hili? Kwa sababu hata hivyo, kinachokufika wewe sasa ni jaribio moja fupi baada ya lingine. Labda sio mfadhaiko mkuu kwako sasa kwa hiyo unaacha mambo yaelekee kwa mwelekeo fulani, sio kuuchukulia kama utajiri wa thamani kwa ufukuziaji wako wa maendeleo.

Ijumaa, 14 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana.

Alhamisi, 13 Juni 2019

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

Jumatano, 12 Juni 2019

Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake.

Jumanne, 11 Juni 2019

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu.

Jumatatu, 10 Juni 2019

Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda.

Ijumaa, 7 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

maneno-ya-Mungu, ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)

Kazi Yangu iko karibu kukamilika. Miaka mingi ambayo tumeshinda pamoja imekuwa kumbukumbu zisizovumilika za siku za nyuma. Nimeendelea kurudia maneno Yangu na Sijakoma kuendelea katika kazi Yangu mpya. Bila shaka, ushauri Wangu ni sehemu muhimu katika kila sehemu ya kazi Ninayoifanya. Bila ushauri Wangu, ninyi nyote mtapotea, na kuchanganyikiwa hata zaidi. Kazi Yangu sasa karibu inakamilika na kuisha; bado Nataka kufanya kazi fulani katika kutoa ushauri, hiyo ni, kutoa baadhi ya maneno ya ushauri ili muyasikilize.

Alhamisi, 6 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (4)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (4)

Amani na furaha Nizungumziayo leo sio sawa na yale ambayo unaamini na kufahamu. Ulikuwa ukifikiri kwamba amani na furaha yalimaanisha kuwa na furaha siku nzima, kutokuwako kwa magonjwa au misiba katika familia yako, kuwa mwenye furaha kila mara ndani ya moyo wako, bila hisia zozote za huzuni, na furaha isiyoelezeka ndani yako haijalishi kiasi cha urefu wa maisha yako mwenyewe. Hilo lilikuwa ni pamoja na nyongeza katika mshahara wa mume wako na mwanao kuingia katika chuo kikuu karibuni.

Jumatano, 5 Juni 2019

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

kumjua mungu, Kazi ya Mungu
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mwanadamu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu.

Jumanne, 4 Juni 2019

Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Maneno ya Mungu, neno la Mungu, siku za mwisho
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo.

Jumatatu, 3 Juni 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Juu ya Hatima

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Juu ya Hatima

Wakati wowote hatima inatajwa, muichukulie kwa uzito maalumu; nyinyi nyote ni mahususi hasa kuhusu jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye kuwa na hatima nzuri. Naweza jishirikisha na hamu yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Kabisa hamtaki miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kuishi kwa uhuru zaidi na kwa urahisi.

Jumapili, 2 Juni 2019

Ni Nini Utambulisho wa Asili wa Mtu na Thamani Yake?

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Watu Waliochaguliwa Nchini China Hawawezi Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Mlitengwa kutoka kwa matope na kwa vyovyote vile, mlichaguliwa kutoka kwa mashapo, wachafu na mliochukiwa na Mungu. Mlikuwa wa Shetani[a] na wakati mmoja mlikanyagwa na kuchafuliwa na yeye. Hii ndiyo maana inasemwa kuwa mlitengwa kutoka kwa matope, na nyinyi si watakatifu, lakini badala yake nyinyi ni vitu visivyo binadamu ambavyo Shetani kwa muda mrefu alikuwa amevifanya vipumbavu. Haya ndiyo maelezo sahihi zaidi yenu.

Jumamosi, 1 Juni 2019

Watu Waliochaguliwa Nchini China Hawawezi Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Neno la Mwenyezi Mungu | Watu Waliochaguliwa Nchini China Hawawezi Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Nyumba ya Daudi ilipokea ahadi ya Bwana, na ilikuwa ni familia iliyopokea urithi wa Yehova. Ilikuwa kwa asili moja ya makabila ya Israeli na ilikuwa ya watu waliochaguliwa. Wakati huo, Yehova aliamuru sheria iwepo kwa Wana wa Israeli kuwa Wayahudi wote waliokuwa wa nyumba ya Daudi, wale wote waliozaliwa katika nyumba hiyo wangepokea urithi Wake. Wangepokea sehemu mia kwa moja na kupata hadhi ya wana wa kiume wazaliwa wa kwanza.